Swali: Ni Tafsiyr ipi iliyosalimika na makosa ambayo unapendekeza?
Jibu: Tafsiyr zilizosalimika na makosa ni nyingi – na himdi zote ni za Allaah. Kubwa na pana katika hizo ni “Tafsiyr Ibn Jariyr” ambaye ndio imamu wa wafasiri wa Qur-aan. Kila aliyekuja baada yake ananukuu kutoka kwake. Kisha kunakuja “Tafsiyr Ibn Kathiyr”, “Tafsiyr al-Baghawiy”, “Tafsiyr as-Sa´diy” ya leo, “Tafsiyr ya Shaykh wetu Muhammad Amiyn ash-Shanqiytwiy. Zote hizi ni – na himdi zote ni za Allaah – Tafsiyr zenye kuaminika zilizojengewa juu ya dalili na juu ya maneno y Salaf.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-2-13.mp3
- Imechapishwa: 19/08/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket