Syria na ´Iraaq hakuna Jihaad – ni fitina

Swali: Unasemaje kuwaambia wanafunzi kuhusiana na fitina hizi zilizotuzunguka na zilizo karibu yetu. Vipi unatakiwa kuwa msimamo wa Muislamu kwazo? Je, ni lazima kuhadithia kila kinachoendelea?

Jibu: Ni lazima kwa mwanafunzi kuwanasihi Waislamu kutoingia katika fitina hizi na kuzijongelea. Wawabainishie lililo la wajibu kwao kwa mnasaba wa fitina na kwamba wajitenge nazo na wamuombe Allaah kinga kwazo. Wawanasihi ndugu zao wasijiingize kwazo wala kwenda huko. Wasisafiri kuziendea yale wanayoita kuwa ni “Jihaad”. Sio Jihaad. Ni fitina. Jihaad ina mpangilio wake unaojulikana katika Uislamu. Yametajwa katika vitabu vya ´Aqiydah jinsi inavyopaswa kupangwa na mtawala na kuiendesha. Jihaad ina hukumu zake zinazojulikana. Hii ni fitina. Sio Jihaad. Ni lazima kwa muislamu ajitenga nazo mbali na awanasihi ndugu zake kujiepusha nazo na kutoingia ndani yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Muntaqaa (96) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/montaqo%20-%204%20-%2011-%201435.mp3
  • Imechapishwa: 19/04/2015