Swali: Ambaye anatenda baadhi ya madhambi makubwa afunge siku ya ´Arafah?

Jibu: Inapendeza kufunga swawm ya ´Arafah ni mamoja kwa ambaye yuko na madhambi makubwa na ambaye hana. Inapendeza kwa kila muislamu kufunga swawm ya ´Arafah. Afanye hivo ili Allaah amfanyie wepesi dhambi zake kutokana na matendo mema.

Swali: Vipi kwa mtenda maasi anayendelea katika maasi yake?

Jibu: Inapendeza kwa kila muislamu kufunga swawm za kujitoela ijapo ni mtenda madhambi. Mtenda dhambi ndiye mtu mwenye haki ya zaidi ya kuyapupia mambo ya kheri. Pengine kwa kufanya hivo akakhafifishiwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22820/ما-حكم-التطوعات-لمن-عنده-بعض-الكباىر
  • Imechapishwa: 26/08/2023