Swawm ya waliofungua robo saa kutokana na adhaana ya kimakosa ya muadhini

Swali: Katika kitongoji kimoja cha ar-Riyaadh mwezi wa Ramadhaan mtukufu hali ya hewa ilikuwa ya mawingu ambapo muadhini akaadhini takriban robo saa kabla ya kufika wakati wa Maghrib pasi na kukusudia na akala kila ambaye alisikia adhaana. Je, wanalazimika kulipa?

Jibu: Ndio. Kikosi cha wanazuoni wengi wanaona kuwa ni lazima kwao kulipa kwa kutokojua kwao. Aidha ni lazima kulipa siku hiyo. Hivi ndivo wanavoona kikosi cha wanazuoni wengi. Ni kama ambavyo watakula asubuhi wakidhani kuwa ni usiku kisha baadaye ikabainika kuwa wamekula wakati wa mchana. Katika hali hiyo watatakiwa walipe siku hiyo. Vilevile ni kama ambavyo watu watakula siku ya tarehe 30 Sha´baan kisha baadaye wakati wa mchana ikathibiti kuwa bado ni Ramadhaan. Katika hali hiyo watatakiwa kujizuilia na baadaye watalazimika kujizuilia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/audios/794/فتاوى-رمضانية
  • Imechapishwa: 01/04/2023