Swali: Amefungua yule ambaye ataapa kwa wingi kipindi cha asubuhi au katika kipindi cha swawm?

Jibu: Kuapa kwa wingi ni dalili ya unyonge wa imani. Miongoni mwa kumtukuza Allaah ni muumini kutoapa kwa wingi. Amesema (Ta´ala):

وَلَا تَجْعَلُوا اللَّـهَ عُرْضَةً لِّأَيْمَانِكُمْ

“Wala msimfanye Allaah kuwa ni nyudhuru ya viapo vyenu.” (02:224)

وَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ

”Chungeni viapo vyenu.” (05:89)

Hapa ni pale ambapo ataapa kwa jina la Allaah akiwa ni mkweli. Kuhusu swawm haiharibiki kwa kuapa kwa wingi. Lakini jambo hilo linaweza kupunguza thawabu zake.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdul-´Aziyz Aalish-Shaykh

´Abdullaah bin Ghudayyaan

Swaalih al-Fawzaan

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (23/139) nr. (18641)
  • Imechapishwa: 28/09/2022