11 – Kumshukuru mume juu ya yale mambo mazuri na wema anaomfanyia. Kushukuru huko kunakuwa kwa maneno mazuri, kumtii katika yaliyo mema na kutosahau wema wake na kujiepusha na ijitihada zake. Kufanya mambo hayo kunapelekea yeye kuingia Motoni. Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nimeonyeshwa Moto na tahamaki nimeona wakazi wake wengi walikuwa ni wanawake.” Wakasema: “Wanakufuru Allaah?” Akasema: Akasema: “Wanakufuru matangamano mazuri na wanakufuru wema. Lau utamtendea mmoja wao wema mwaka mzima na halafu katika tokeo fulani akaona kitu kwako, atasema: “Katu sijaona wema wowote kutoka kwako.”[1]

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah hamtazami mwanamke ambaye hamshukuru mume wake wakati huohuo hawezi kujitosheleza naye [kukosa kuwa pamoja naye].”[2]

[1] al-Bukhaariy (01/83, 528) na (02/232, 540), (06/297) na (09/298 – Fath) na Muslim (907) na wengineo.

[2] Silsilah Ahaadiyth-is-Swahiyhah, uk. 289.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad Shuwmaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifaat-uz-Zawjah as-Swaalihah, uk. 33-34
  • Imechapishwa: 28/09/2022