19. Mke mwema anajaribu kumfurahisha mume kwa hali zote

13 – Mke mwema anajaribu kumfurahisha mume kwa njia ziwezekanazo. Tumekwishatangulia kutaja katika Hadiyth maneno ya mwanamke mwema:

“Mimi leo sionji usingizi mpaka uridhie.“[1]

adh-Dhahabiy amesema:

“Ni lazima kwa mwanamke atafute kumridhisha na kumfurahisha mume wake na ajiepushe na kumkasirisha. Asijizuilie kutokana naye pale atapomuhitaji. Vilevile mwanamke anatakiwa kujua kuwa yeye ni kama mmlikiwa wa mume. Asifanye chochote kwa nafsi yake wala mali yake mume isipokuwa kwa idhini yake. Amtangulizie haki yake mume kabla ya haki yake yeye na pia atangulize mbele haki za jamaa zake mume kabla ya haki za jamaa zake yeye na mwanamke awe mwenye kujiandaa kwa mume kustarehe naye kwa sampuli zote za usafi na wala asijifakharishe kwake kutokana na uzuri wake. Asimtie kasoro kwa ubaya – ikiwa mume ana ubaya huo.

Vilevile ni lazima kwa mwanamke siku zote amuonee hayaa mume wake, asimkodolee macho, kumtii amri zake, kunyazama wakati anapozungumza, kujiepusha na yale yote yanayomkasirisha na kutomfanyia khiyana wakati  wa kutokuwepo kwake katika kitanda chake na mali yake na nyumba yake. Aidha anukie hafuru nzuri, auzoweze mdomo kutumia Siwaak, miski na manukato. Adumu kuvaa mapambo anapokuwa mbele yake na aache kujipamba mume anapokuwa hayupo, akawakirimu familia na jamaa zake mume na akione kidogo kinachotoka kwake kuwa ni kikubwa.”[2]

[1] Silsilah Ahaadiyth-is-Swahiyhah, uk. 287.

[2] al-Kabaair, uk. 188-190 kwa kifupi.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad Shuwmaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifaat-uz-Zawjah as-Swaalihah, uk. 35-36
  • Imechapishwa: 28/09/2022