Swali: Kuna mwanamke ambaye siku moja alifunga. Baada ya kukata kwake swawm kwa tende na maji lakini kabla ya kuswali Maghrib ndipo ikamjia ada yake ya mwezi. Je, swawm yake ya siku hiyo imesihi au aifunge tena?

Jibu: Ikiwa ameona damu baada ya kuzama kwa jua na baada ya kukata swawm, ijapo kwa maji tu, muhimu ni baada ya kuzama kwa jua, basi funga yake ni sahihi. Haijalishi kitu hata kama ada yake imemjia kabla ya yeye kuswali Maghrib. Muda wa kuwa jua limekwishazama kabla ya ada kumjilia na kabla ya damu kutoka, basi swawm yake ni sahihi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4835/حكم-من-اتتها-العادة-الشهرية-مع-وقت-الافطار
  • Imechapishwa: 26/03/2023