Swawm ya ambaye amelala kabla ya kufungua na akaamka alfajiri siku inayofuata

Swali: Mtu akilala kabla ya futari na asiamke isipokuwa asubuhi ya siku inayofuata – je, aendelee na swawm yake au afungue?

Jibu: Aendelee na swawm yake. Hayo yalimtokea Qays bin Swirmah. Alikuwa kufanya kazi ngumu na hapo mwanzoni wakati ilipofaradhishwa swawm ilikuwa ukilala usiku kabla ya kufungua basi huhalalikiwi tena na chakula. Akarudi kwa mke wake na kuuliza: “Je, kuna chakula?” Akajibu: “Hapana, lakini hebu wacha nende kukutafutia chakula.” Aliporudi akamkuta amelala ambapo akasema maneno yenye maana: “Umekula patupu na umekhasirika.” Baada ya hapo Qays akaondoka na kufanya kazi mpaka nusu ya mchana ambapo akazimia. Ndipo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) akateremsha Aayah isemayo:

أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَائِكُمْ ۚ هُنَّ لِبَاسٌ لَّكُمْ وَأَنتُمْ لِبَاسٌ لَّهُنَّ ۗ عَلِمَ اللَّـهُ أَنَّكُمْ كُنتُمْ تَخْتَانُونَ أَنفُسَكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ وَعَفَا عَنكُمْ ۖ فَالْآنَ بَاشِرُوهُنَّ وَابْتَغُوا مَا كَتَبَ اللَّـهُ لَكُمْ ۚ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ

“Mmehalalishiwa usiku wa swawm kujamiiana na wake zenu; wao ni vazi kwenu na nyinyi ni vazi kwao. Allaah anajua kwamba nyinyi mlikuwa mkizihini nafsi zenu hivyo akapokea tawbah yenu na akakusameheni. Basi sasa changanyikeni nao [waingilieni] na tafuteni Aliyokuandikieni Allaah kwenu. Kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni swawm mpaka usiku.”[1]

[1] 02:187

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaaih wa Naswaaih, uk. 75-76
  • Imechapishwa: 17/03/2024