Swawm sio sharti ya I´tikaaf

Swali: Je, I´tikaaf inashurutisha mtu afunge?

Jibu: Haishurutishi. Hii ni miongoni mwa dalili ya kutoshurutishwa kufunga. Kwa sababu usiku sio wakati wa kufunga. Kwa ajili hiyo Ibn ´Abbaas amesema.

“Sio lazima kwa mwenye kukaa I´tikaaf afunge, isipokuwa akijilazimisha nayo mwenyewe.”

Hata hivyo bora ni mtu afunge pia akiweza kufanya hivo wakati wa mchana.

Swali: Ni yepi majibu juu ya Hadiyth hii wale wenye kuona kuwa ni sharti kwa mwenye kukaa I´tikaaf kufunga?

Jibu: Hawana dalili. Pengine wanajengea hoja kwa masimulizi ya ´Aaishah aliposema:

“Hakuna I´tikaaf isipokuwa kwa kufunga.”

Hata hivyo maneno ya ´Aaishah yanapingana na maneno ya Ibn ´Abbaas. Msingi ni kutokuwepo sharti.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23821/هل-يشترط-الصوم-في-الاعتكاف
  • Imechapishwa: 15/05/2024