Mwenye kukaa I´tikaaf ajishughulishe na nini zaidi?

Swali: Lipi bora kwa mwenye kukaa I´tikaaf ajishughulishe na ´ibaadah au elimu?

Jibu: Kusoma, darsa na usomaji wa vitabu ni katika ´ibaadah. Ajishughulishe na yale ambayo Allaah amemsahilishia katika yale ambayo yanamchangamsha zaidi na kufanya moyo wake kuwa na unyenyekevu zaidi. Mara aswali, mara amtaje Allaah, mara asome Qur-aan, mara asome vitabu vya elimu na Hadiyth. Atazame kile chenye manufaa, chenye faida na chenye kufanya moyo wake kuwa na unyenyekevu zaidi. Yote haya ni katika ´ibaadah. Kama kuna vikao vya elimu avihudhurie.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23820/هل-اشتغال-المعتكف-بالعبادة-افضل-ام-العلم
  • Imechapishwa: 15/05/2024