Swali: Je, anayeacha swalah aamrishwe kuswali? Akifunga swawm yake ina nafasi?

Jibu: Mwenye kuacha swalah ni kafiri. Kafiri hana swawm ingawa atachukuliwa hatua na kuadhibiwa juu ya hilo siku ya Qiyaamah. Makafiri wanazungumzishwa tanzu za Shari´ah kwa njia ya kuwaadhibu. Lakini watatakiwa kufanya mambo hayo baada ya kuingia katika Uislamu. Kwa ajili hiyo wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomwagiza Mu´aadh kwenda Yemen alimwamrisha awaamrishe kwanza Tawhiyd, kisha swalah, kisha zakaah. Kafiri anaanza kuamrishwa shahaadah. Akisilimu ndio anaamrishwa swalah, zakaah, swawm na mambo mengine. Ambaye anaacha swalah amefanya kichenguzi miongoni mwa vichenguzi vya Uislamu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kati ya mtu na ukafiri na shirki ni kuacha swalah.”

“Ahadi iliopo kati yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi, yule mwenye kuiacha amekufuru.”

“Yule mwenye kuacha swalah ya ´Aswr matendo yake yameporomoka.”

Hana swawm yoyote mpaka atubie kwa Allaah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/audios/794/فتاوى-رمضانية
  • Imechapishwa: 01/04/2023