Swalah ya Witr inatofautiana na swalah ya usiku?

Swali: Je, swalah ya Witr inatofautiana na swalah ya Witr inapokuja katika wakati wake na du´aa inayoombwa katika Rak´ah mbili na vivyo hivyo idadi ya Rak´ah za swalah?

Jibu: Witr ni katika swalah ya usiku. Nayo ni Sunnah. Nayo ndio ya kumalizia. Ni Rak´ah moja ambayo mtu anamalizia swalah ya usiku mwishoni mwa usiku, katikati ya usiku au mwanzoni mwa usiku baada ya swalah ya ´Ishaa. Ataswali kile atachoweza kisha atamalizia kwa Rak´ah moja ambayo ndani yake ataswali al-Faatihah na Qul huwa Allaahu ahadu. Hii ndio Witr. Mtume  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ifanyeni swalah yenu ya mwisho usiku ni Witr.”[1]

Atasoma ndani yake baada ya Rukuu´ du´aa iliopokelewa:

اللهم اهدني فيمن هديت, وعافني فيمن عافيت, وتولني فيمن توليت, وبارك لي فيما أعطيت, وقني شر ما قضيت, فإنك تقضي ولا يقضى عليك, وإنه لا يذلّ من واليتَ, ولا يعزّ من عاديت, تباركت ربنا وتعاليت، لا منجا منك إلا إليك

“Ee Allaah! Niongoze pamoja na wale Uliowaongoza, uniafu pamoja na wale Uliowaafu, Uniangalie pamoja na wale Unaowaangalia, Unibariki katika kile Ulichotoa na Unilinde kutokamana na shari kwa yale Uliyohukumu. Kwani hakika Wewe ndiye mwenye kuhukumu na wala Huhukumiwi. Hakika hatwezeki yule Uliyemfanya mpenzi na wala hapati nguvu yule Uliyemfanya adui. Umebarikika na Umetukuka Mola wetu. Hakuna mahali pa kuokoka kutokamana na Wewe isipokuwa Kwako.”

Ni du´aa ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimfunza al-Hasan bin ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Aombe pamoja nayo kile kitachomkuia chepesi miongoni mwa du´aa nzuri.

[1] al-Bukhaariy (452) na (943) na Muslim (1245).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/309)
  • Imechapishwa: 04/11/2021