Aswali vipi aliyeswali Witr mwanzoni mwa usiku akaamka tena usiku?

Swali: Vipi niswali endapo nitaswali Witr mwanzoni mwa usiku kisha nikaamka kuswali mwishoni mwa usiku?

Jibu: Ukiswali Witr mwanzoni mwa usiku kisha Allaah akamfanyia wepesi wa kusimama mwishoni mwake, basi aswali yale ambayo Allaah amekufanyia wepesi shufwa pasi na Witr tena. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna Witr mbili katika usiku mmoja.”

Pia imethibiti kupitia kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiswali Rak´ah mbili baada ya Witr hali ya kuwa ameketi chini. Hekima ya hilo – Allaah ndiye mjuzi zaidi – ni kuwabainishia watu kufaa kuswali baada ya Witr.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/311)
  • Imechapishwa: 04/11/2021