Swali: Kuna mtu na watoto wake wamepitwa na swalah ambapo akasimama yeye na mtoto wake mmoja akasimama upande wa kulia na mwingine upande wa kushoto. Akaja mtu kwa nyuma akamvuta yule mtoto. Baada ya swalah yule mtu akamkemea baba na kumwambia kuwa kitendo hichi hakijuzu kwa kuwa mtoto hajabaleghe. Ni sahihi?

Jibu: Hili si sahihi. Watoto maadamu wana upeo wa upambanuzi basi wanaweza kusimama nyuma yake. Hakuna neno. Swalah yao ni sahihi, kwa kuwa wana uwezo wa kupambanua. Waswali nyuma yake. Amekosea katika hili. Kadhalika ni sawa wakisimama upande wa kulia na wa kushoto kwa imamu. Njia zote mbili zinajuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (19) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf%2030-7-1434_01.mp3
  • Imechapishwa: 15/06/2020