Swalah ya Tarawiyh ni mkusanyiko

Swali: Kuna profesa ambaye kasema kuwa swalah ya Tarawiyh haiwi kwa mkusanyiko.

Jibu: Sunnah katika swalah ya Tarawiyh iswaliwe msikitini mkusanyiko. Hivo ndivo alivofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika baadhi ya nyusiku mwezi wa Ramadhaan. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaswalisha Maswahabah nyusiku tatu na usiku wa nne (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakutoka na akasema:

“Nimechelea isije kufaradhishwa kwenu.”

Wakati wa uongozi wa ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) aliwaona watu wanaswali kila mmoja akiswali kivyake ambapo akasema:

“Lau ningewakusanya nyuma ya imamu mmoja.”

Akamwamrisha Ubayy awaswalishe watu. Sababu iliyomzuia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuendelea na swalah ya Tarawiyh imekwishaondoka. Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) wameafikiana juu ya kile alichoona ´Umar na wakaona kuwa kitendo hicho ni kuhuisha Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hakuna mwanachuoni yeyote wa Kiislamu, hapo zamani na hivi sasa, ambaye ameonelea kinyume na hivo.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdullaah bin Ghudayyaan

Swaalih al-Fawzaan

´Abdul-´Aziyz Aalish-Shaykh

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (06/80) nr. (17882)
  • Imechapishwa: 22/04/2022