Imamu asubiri mkusanyiko wa pili au aanze Tarawiyh?

Swali: Je, inafaa kwa imamu kusimama kuswali Tarawiyh licha ya kwamba kuna kikosi cha watu wanaoswali ´Ishaa mkusanyiko wa pili?

Jibu: Hapana kizuizi imamu akasimama kuswali Tarawiyh baada ya kumaliza kuswali ´Ishaa na Raatibah yake hata kama kuna kikosi cha watu wanaoswali. Kwa sababu ´Ishaa imeshawapita pamoja na imamu. Inafaa kwao pia kuswali pamoja na imamu ambaye anaswali Tarawiyh na wakati huohuo wao wamenuia swalah ya ´Ishaa. Pindi imamu atatoa salamu watasimama na kukamilisha swalah zao kivyao. Vilevile wanaweza kuswali mkusanyiko peke yao maeneo ambapo hakuna tashwishi juu yao na kwa imamu.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (06/81) nr. (20795)
  • Imechapishwa: 22/04/2022