Swalah ya msafiri kabla ya safari na baada ya kurudi mji wake

Swali: Kukiadhiniwa na msafiri akawa bado ndani ya mji kisha akataka kusafiri – Je, inafaa kwake kufupisha?

Jibu: Anaweza kusafiri na kuiswali akiwa safarini. Iwapo adhaana ya Dhuhr itaadhiniwa, kisha akatoka na akaiswali akiwa safarini, ataswali kwa kufupisha. Kinachozingatiwa ni ule wakati wa kitendo. Vivyo hivyo ikiwa ataingia katika mji, akaingia katika nchi yake na akawa bado hajaswali, basi ataswali Rak´ah nne, hata kama wakati wa swalah uliingia akiwa safarini. Mfano kama wakati wa Dhuhr ulimfikia akiwa safarini na akafika hali ya kuwa hajaswali, ataswali Rak´ah nne. Au kumeadhiniwa akiwa katika mji wake kisha akatoka na akaiswali akiwa safarini, ataswali Rak´ah mbili.

Mwanafunzi: Maana yake kigezo ni ule wakati wa kutekeleza swalah?

Ibn Baaz: Wakati wa kuitenda.

Mwanafunzi: Kama yule aliyekumbuka swalah ya safari akiwa nyumbani?

Ibn Baaz: Ataswali Rak´ah nne, kwa sababu udhuru umekwisha.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31545/هل-يقصر-المسافر-الصلاة-اذا-اذن-قبل-السفر
  • Imechapishwa: 01/11/2025