Swali: Kumekimiwa swalah punde tu baada ya adhaana.

Jibu: Sunnah ni kwamba Iqaamaha iwe baada ya adhaana kwa muda fulani ili watu wapate nafasi ya kuswali Raatibah za Fajr na za Dhuhr, Rak´ah mbili kabla ya ´Aswr, Rak´ah mbili kabla ya Maghrib. Asifanye haraka. Kuwepo muda wa kati yao ili waliopo wapate kuswali Sunnah ya Fajr, Sunnah ya Dhuhr, Rak´ah mbili kabla ya Maghrib na Rak´ah mbili kabla ya ´Ishaa. Hivyo Sunnah ni kutofanya haraka.

Swali: Je, muda wa kati yao unapangwa vipi?

Jibu: Hakuna muda maalum. Muda mfupi unatosha, kama robo saa au theluthi saa. Kitu cha kukaribiana hivyo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31549/ما-حكم-عدم-الفصل-بين-الاذان-والاقامة
  • Imechapishwa: 01/11/2025