Swalah ya mkusanyiko kwa anayesukumwa kwenye kiti cha magurudumu

Swali: Kuna bwana mmoja anaketi kwenye kiti cha magurudumu. Je, analazimika kumwajiri mtu ambaye atamsukuma ili aweze kuhudhuria swalah?

Jibu: Kinachonidhihirikia ni kwamba inafaa kwake kuswali nyumbani. Lakini akitarajia malipo ni sawa. Yuko na udhuru unaokubalika Kishari´ah. Hata hivyo akitarajia malipo ni kama alivosema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“… wangeziendea ijapo kwa kutambaa.”[1]

Swali: Je, mtu anaweza kusema kwamba ambacho kinahitajika ili kukamilisha wajibu basi nacho kinakuwa wajibu?

Jibu: Naona kuwa hakumlazimu.

[1] Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalah nzito zaidi kwa wanafiki ni swalah ya ´Ishaa na swalah ya Fajr. Endapo wangelijua yale yanayopatikana ndani yake basi wangeziendea ijapo kwa kutambaa.” (al-Bukhaariy na Muslim)

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23731/هل-يلزم-المقعد-استىجار-من-يقوده-الى-الصلاة
  • Imechapishwa: 18/04/2024