Imamu ameswali kwa Rak´ah pungufu na anachelea asiwatatize wajinga

Swali: Imamu akiswali Rak´ah mbili kisha akakumbushwa na akachelea wasitatizwe watu wasiokuwa na elimu na hivyo akawaambia kwamba ataswali Rak´ah mbili na atasujudu mara mbili ili asiwatatize.

Jibu: Aswali zilizobakia na hana haja. Yanatosha yale aliyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Asimame na aswali yale yaliyobakia na wala asiseme kitu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23738/حكم-امام-سها-وخشي-التلبيس-على-المصلين
  • Imechapishwa: 18/04/2024