Sunnah kwa imamu kabla ya kuanza kuswalisha

Swali: Ni ipi hukumu ya imamu asiyegeuza kuliani wala kushotoni?

Jibu: Sunnah kwa imamu ni yeye akague kuliani na kushotoni na awahimize kusawazisha safu na wazibe upenyo na zianze kukamilishwa zile safu zilizoko mbele kwanza ili kupatikane nafasi katika zile zilizoko nyuma. Awazindue watu na asighafilike ili watu wazinduke kuifanyia kazi Sunnah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23739/هل-من-السنة-التفات-الامام-لتسوية-الصفوف
  • Imechapishwa: 18/04/2024