ar-Raajihiy: Je, ikiwa kupatwa kwa jua kutatokea baada ya swalah ya Fajr kuswaliwe?
Jibu: Kuswaliwe kwa sababu bado wakati wake uko ndani ya mamlaka ya kuswali, kwani jua bado halijachomoza. Hilo ni kutokana na kuenea kwa dalili. Isitoshe mwaka huu tuliswali Twaa-if wakati mwezi ulipatwa pamoja na alfajiri, na pia tukaswali baada ya kuchomoza kwa alfajiri.
ar-Raajihiy: Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) amesema:
“Na dalili sahihi zinaonesha kwamba makatazo ya kuswali wakati wa alfajiri hayahusiani moja kwa moja na kuchomoza kwake”?
Jibu: Kuna hoja zinazoweza kupingwa hapa; kwa sababu kupatwa kwa mwezi baada ya swalah ya Subh hakuzuia kuswali kabla ya Subh. Dalili nyingine zinafahamisha kuwa kabla ya Subh pia ni wakati wa makatazo, isipokuwa kwa ajili ya Sunnah ya Fajr. Hali hii ni tofauti na swalah ya ´Aswr, ambapo wakati wa makatazo hauingii isipokuwa kwa yule aliyekwishaswali ´Aswr. Kwa mfano ikiwa mtu yuko safarini na hakuswali hadi baada ya watu wengine kuswali, au mgonjwa ambaye hakuweza kuswali mpaka baada ya watu wengine, basi hakumzuii mtu kuswali swalah ya kujitolea kabla ya swalah ya faradhi. Katika hali hii mtu ataswali swalah ya kujitolea kwanza, kisha ataswali faradhi. Hivyo basi wakati wa makatazo huanza kwake baada ya kuswali ´Aswr, si baada ya watu wengine kuswali, bali baada ya yeye mwenyewe kuswali.
ar-Raajihiy: Je, maneno yake yanayosema kwamba hali ya Fajr ni sawa na ´Aswr yana usahihi gani?
Jibu: Maoni sahihi ni kwamba si sawa na ´Aswr. Wakati wa makatazo huanza baada ya kuchomoza Fajr. Hakuna kinachobaguliwa katika hayo isipokuwa Sunnah ya Fajr na swalah ya mamkuzi ya msikiti peke yake.
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24889/حكم-صلاة-الكسوف-اذا-كان-بعد-الفجر
- Imechapishwa: 30/12/2024
ar-Raajihiy: Je, ikiwa kupatwa kwa jua kutatokea baada ya swalah ya Fajr kuswaliwe?
Jibu: Kuswaliwe kwa sababu bado wakati wake uko ndani ya mamlaka ya kuswali, kwani jua bado halijachomoza. Hilo ni kutokana na kuenea kwa dalili. Isitoshe mwaka huu tuliswali Twaa-if wakati mwezi ulipatwa pamoja na alfajiri, na pia tukaswali baada ya kuchomoza kwa alfajiri.
ar-Raajihiy: Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) amesema:
“Na dalili sahihi zinaonesha kwamba makatazo ya kuswali wakati wa alfajiri hayahusiani moja kwa moja na kuchomoza kwake”?
Jibu: Kuna hoja zinazoweza kupingwa hapa; kwa sababu kupatwa kwa mwezi baada ya swalah ya Subh hakuzuia kuswali kabla ya Subh. Dalili nyingine zinafahamisha kuwa kabla ya Subh pia ni wakati wa makatazo, isipokuwa kwa ajili ya Sunnah ya Fajr. Hali hii ni tofauti na swalah ya ´Aswr, ambapo wakati wa makatazo hauingii isipokuwa kwa yule aliyekwishaswali ´Aswr. Kwa mfano ikiwa mtu yuko safarini na hakuswali hadi baada ya watu wengine kuswali, au mgonjwa ambaye hakuweza kuswali mpaka baada ya watu wengine, basi hakumzuii mtu kuswali swalah ya kujitolea kabla ya swalah ya faradhi. Katika hali hii mtu ataswali swalah ya kujitolea kwanza, kisha ataswali faradhi. Hivyo basi wakati wa makatazo huanza kwake baada ya kuswali ´Aswr, si baada ya watu wengine kuswali, bali baada ya yeye mwenyewe kuswali.
ar-Raajihiy: Je, maneno yake yanayosema kwamba hali ya Fajr ni sawa na ´Aswr yana usahihi gani?
Jibu: Maoni sahihi ni kwamba si sawa na ´Aswr. Wakati wa makatazo huanza baada ya kuchomoza Fajr. Hakuna kinachobaguliwa katika hayo isipokuwa Sunnah ya Fajr na swalah ya mamkuzi ya msikiti peke yake.
Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24889/حكم-صلاة-الكسوف-اذا-كان-بعد-الفجر
Imechapishwa: 30/12/2024
https://firqatunnajia.com/swalah-ya-kupatwa-kwa-jua-katika-nyakati-uliyokatazwa-kuswali/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)