Sujuud kabla au baada ya salamu inahusiana na ubora

Swali: Je, Sujuud ya kusahau inakuwa kabla au baada ya salamu?

Jibu: Inahusiana na ubora tu. Lakini bora zaidi ni kwamba ikiwa mtu amesalimu huku akiwa amepunguza, basi katika hali hiyo asujudu baada ya salamu. Vivyo hivyo ikiwa amejengea juu ya dhana yake kubwa, Sujuud inakuwa baada ya salamu. Kwa hali nyingine zote Sujuud inakuwa kabla ya salamu. Hata hivyo ikiwa mtu atafanya sijda baada ya salamu kwa hali ambayo bora ingekuwa kabla ya salamu, au akafanya sijda kabla ya salamu kwa hali ambayo bora ingekuwa baada ya salamu, hiyo bado itakuwa sahihi na hakuna tatizo. Hadiyth sahihi zinajulisha juu ya sura hiyo. Kwa hivyo kuzioanisha zote ni ubora huu. Kwa hivyo itasihi endapo atasujudu kabla ya salamu baada ya kupunguza kitu. Kwa mfano atasahau Tashahhud ya kwanza na akaichelewesha na kusujudu baada ya salamu, hapana vibaya. Inahusiana na ubora tu. Ubora unahusiana na kuzingatia yale aliyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Swali: Je, atatakiwa kusema ”Allaahu Akbar”?

Jibu: Ndio, anapaswa kusema ”Allaahu Akbar”. Ataleta Takbiyr wakati wa kusujudu na wakati wa kuinuka. Hivi ndivo imepokelewa katika Hadiyth ya Abu Hurayrah na Hadiyth ya ´Imraan.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24893/متى-يكون-سجود-السهو-قبل-السلام-ومتى-بعده
  • Imechapishwa: 30/12/2024