Swalah ya jeneza tu ndio inajuzu makaburini

Swali: Wakati mwingine makaburini kunawekwa jeneza kati ya makaburi kisha wanaliswalia wale ambao hawajaliswalia. Je, kitendo hichi ni sahihi?

Jibu: Ndio. Swalah ya jeneza makaburini ni sawa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya hivo pale aliposwalia kaburi. Pindi alipokuwa hajaliswalia kabla ya kuzikwa akaliswalia. Hili linahusiana tu na swalah ya jeneza. Ama kuhusu swalah nyenginezo haijuzu kuziswali kwenye makaburi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (27) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2139
  • Imechapishwa: 12/07/2020