Kuchinja kwa ajili ya Allaah kwenye kaburi la al-Badawiy

Swali: Mwenye kusema kuwa anachinja kwa ajili ya Allaah na anakiri ya kwamba kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah ni shirki lakini anachinja kwenye kaburi la al-Badawiy kwa kuwa kufanya hivyo kuko karibu na kukubaliwa. Ni ipi hukumu ya kitendo hichi?

Jibu: Hii ni Bid´ah na ni njia inayopelekea katika shirki. Ikiwa unachinja kwa ajili ya Allaah chinja nyumbani kwako kwa ajili ya Allaah au sehemu kwengine popote. Ni kwa nini tu mpaka wende kwenye kaburi la al-Badawiy? Huku ni kujifananisha na wale wenye kuliabudu na kulichinjia na ni kushirikiana nao. Kitendo hichi ni katika njia zinazopelekea katika shirki.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (27) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2139
  • Imechapishwa: 12/07/2020