Swalah ya ambaye amesahau Takbiyrat-ul-Ihraam

Swali: Mtu anayekuja njiani na akakuta kuna kikosi cha watu wanaswali na akajiunga kwa nia ya kuswali pamoja nao. Lakini hata hivyo akasahau kuleta Takbiyrat-ul-Ihraam na asikumbuke hilo isipokuwa katika Rak´ah ya pili. Je, swalah yake ni sahihi au ni batili kwa sababau amesahau nguzo [ya swalah]?

Jibu: Swalah iliyokusudiwa sio sahihi. Kwa sababu hakuleta Takbiyrat-ul-Ihraam ambayo ni nguzo kwa maafikiano ya waislamu. Swalah haifunguki isipokuwa kwayo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/273)
  • Imechapishwa: 31/10/2021