Swali: Swalah inasihi nyuma ya mvuta sigara?

Jibu: Swalah inasihi nyuma ya watenda madhambi wote kwa mujibu wa maoni sahihi. Ibn ´Umar aliswali nyuma ya al-Hajjaaj ambaye ni miongoni mwa watu madhalimu zaidi inapokuja katika mauaji. Hata hivyo kilicho cha wajibu wasimamie wema na si madhalimu pale ambapo kuna uwezekano wa kufanya hivo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24248/حكم-الصلاة-خلف-صاحب-الدخان
  • Imechapishwa: 18/09/2024