Swalah ambayo imeingia mwanamke akiwa na damu

Swali: Baadhi ya wanawake hujifungua baada ya kwamba umeshaingia muda wa swalah. Je, baada ya kutwahirika analazimika kulipa swalah ile ambayo ulifika wakati wake kabla ya yeye kuiswali?

Jibu: Halazimiki kuilipa ikiwa hakuzembea. Lakini ikiwa aliichelewesha mpaka wakati ukawa mfinyu kisha ndio akajifungua, basi atailipa baada ya kusafika kutoka katika damu ya uzazi. Mwanamke huyu ni kama mfano wa mwanamke mwenye hedhi akichelewesha swalah mpaka mwisho wa wakati wake kisha akapata hedhi. Mwanamke huyu anatakiwa kuilipa baada ya kusafika kwa sababu alizembea kwa kule kuichelewesha.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/229)
  • Imechapishwa: 09/09/2021