Swali: Je, ni sahihi ya kwamba kijana kabla ya kutafuta elimu kwanza afanye ´ibaadah kwa wingi kisha baada ya kujishughulisha na ´ibaadah ndio atafute elimu?
Jibu: Haya ni maneno ya Suufiyyah. Wao ndio husema mtu asitafute elimu na badala yake ajishughulishe na ´ibaadah kwa kuwa makusudio ni ´ibaadah. Wanasema mtu ajishughulishe na ´ibaadah na si kutafuta elimu. Baadhi yao pia husema mtu akijishughulisha na ´ibaadah elimu humteremkia bila ya kusoma! Haya ni maneno ya kipotefu. Haya ni maneno ya wapotevu – tunaomba kinga kwa Allaah.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (25) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1428-3-28.mp3
- Imechapishwa: 19/08/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)