Swali: Je, ni sahihi ya kwamba kijana kabla ya kutafuta elimu kwanza afanye ´ibaadah kwa wingi kisha baada ya kujishughulisha na ´ibaadah ndio atafute elimu?

Jibu: Haya ni maneno ya Suufiyyah. Wao ndio husema mtu asitafute elimu na badala yake ajishughulishe na ´ibaadah kwa kuwa makusudio ni ´ibaadah. Wanasema mtu ajishughulishe na ´ibaadah na si kutafuta elimu. Baadhi yao pia husema mtu akijishughulisha na ´ibaadah elimu humteremkia bila ya kusoma! Haya ni maneno ya kipotefu. Haya ni maneno ya wapotevu – tunaomba kinga kwa Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (25) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1428-3-28.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020