Suufiy ndiye aliwazamisha watu wa Nuuh na akawaangamiza kina ´Aad na Thamuud

Faqiyh Abu ´Aliy bin al-Bannaa´ amesema:

“al-Hallaaj alikuwa akidai kuwa ni mungu na akisema kuwa uungu umekita ndani ya mwanadamu. Pindi waziri ´Aliy bin ´Iysaa alipomleta akamuona kuwa mtu huyo hamairi vizuri si Qur-aan, Fiqh wala Hadiyth. Bora kwako ni wewe kujifunza mambo ya faradhi na ya twahara kuliko kuandika mambo ambayo hutambui chochote juu yake. Ole wako! Ni mara ngapi unawaandikia watu: “Ametukuka ambaye ana mwanga wa kung´ara!” Hakika una haja kubwa ya adabu.” Baada ya hapo akaamrisha asubulubiwe, mara ya kwanza alisulubiwa upande wa mashariki na kisha baadaye akasulubiwa upande wa magharibi. Ilipatikana katika vitabu vyake ameandika:

“Mimi ndiye niliwazamisha watu wa Nuuh, mimi ndiye nimewaangamiza kina ´Aad na Thamuud.”

Alikuwa akiwaambia wafuasi wake:

“Wewe ndiye Nuuh, wewe ndiye Muusa na wewe ndiye Muhammad.”

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (14/327)
  • Imechapishwa: 16/11/2020