Alifanya mchezo na swalah miaka ya nyuma baada ya kubaleghe

Swali: Ni ipi hukumu katika Uislamu ya msichana ambaye amefikisha miaka kumi na nne na hakuwa anaswali?

Jibu: Swali hili tunaweza kusema kwamba ni sehemu ya lile swali la kwanza[1]. Msichana huyu ambaye ameacha swalah akiwa na miaka kumi na nne, ikiwa aliacha kwa makusudi pasi na udhuru wa Kishari´ah, basi kutokana na yale tuliyoyapa nguvu ni kwamba hakumfai kitu kulipa ijapokuwa ataswali mara elfumoja. Ni lazima kwake kutubia tawbah ya kweli na akithirishe matendo mema ili Allaah amfutie madhambi makubwa haya aliyofanya. Lakini kujengea maoni ya wanachuoni wengi ni kwamba ni lazima kwake kulipa kila swalah baada ya kubaleghe kwake. Kila swalah aliyoacha baada ya kubaleghe basi ni lazima kwake kuilipa. Hivi ndivo wanavoona wanachuoni wengi. Ni mamoja aliiacha kwa makusudi au kwa udhuru wa Kishari´ah. Lakini maoni sahihi tuliyochagua ni kwamba akiwa aliacha kwa makusudi pasi na udhuru wa Kishari´ah basi hatoilipa. Kwa sababu hakumfai kitu kuikidhi. Kubaleghe kwa mwanamke kunapatikana kwa moja katika mambo mane:

1- Kutokwa na manii.

2- Kuota nywele sehemu za siri.

3- Kufikisha miaka kumi na tano kwa mujibu wa maoni yenye nguvu.

4- Kupata hedhi.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/ni-lini-inalipwa-swalah-iliyompita-mtu/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (10) http://binothaimeen.net/content/6733
  • Imechapishwa: 16/11/2020