Swali: Ipi hukumu ya kuwatahiri wasichana? Kwetu ni lazima tufanye hivyo, na kuna baadhi ya watu wamenambia kuwa ni jambo lisilojuzu kwa kuwa ndani yake kuna kama kuadhibu. Ipi hukumu ya hilo?

Ibn Baaz: Kutahiriwa (kwa wanawake) ni Sunnah iliyosisitizwa, hali kadhalika kwa wanaume, wote ni Sunnah iliyosisitizwa. Na kuna kundi la wanachuoni ambao wanaona ni wajibu kwa wanaume na ndio kauli yenye nguvu. Inatakikana kuwatahiri wanaume na wala haitakikani kulichukulia sahali, na namna hii ni kuwa imependekezwa kuwatahiri wanawake ikiwa atapatikana mwenye kujua hilo katika wanawake wanaotahiri.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Nuur ´alaad-Darb (770)
  • Imechapishwa: 13/03/2018