Swali: Mtu anaweka paji lake la uso ardhini bila pua kugusa chini. Wakati mwingine hata paji la uso haligusi vizuri ardhi. Ni ipi hukumu ya swalah yake?

Jibu: Ni lazima kumakinisha paji la uso na pua ardhini. Sujuud haisihi isipokuwa mpaka hivo. Akikusudia hivo basi swalah yake inabatilika. Ikiwa ni kwa kusahau inabatilika ile Rak´ah aliyofanya hivo na itasimama Rak´ah nyingine mahali pake. Kwa maana nyingine atatakiwa kuleta Rak´ah nyingine ikiwa anaswali peke yake. Akiwa anaswali nyuma ya mtu basi pale ataswali Rak´ah nyingine pale atakaposimama imamu wake, kwa sababu amepoteza Rak´ah moja.

Swali: Vipi ikiwa pua yake haikugusa ardhini Sujuud nzima au imegusa ardhi sehemu ya Sujuud?

Jibu: Ni lazima asujudu juu ya pua na paji la uso vyote viwili. Ni lazima vyote viwili viguse ardhini. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisujudu juu ya paji la uso na pua na akisema:

“Nimeamrishwa kusujudu juu ya viungo saba” ambapo moja wapo ni paji la uso.”

akiashiria kwenye pua.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22732/حكم-عدم-تمكين-الانف-والجبهة-في-السجود
  • Imechapishwa: 09/08/2023