Pindi imamu anaposikia mwenye kuingia msikitini

Swali: Je, imamu anaposikia mtu anaingia msikitini arefushe swalah kiasi ili mtu huyo aweze kuwahi kujiunga na mkusanyiko?

Jibu: Ndio, ndio bora. Arefushe kiasi fulani kiasi kisichowatia uzito watu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anaenda katika Rukuu´ pale ambapo hasikii tena nyayo za miguu. Kwa maana nyingine anamzingatia yule mwingiaji ili aweze kuwahi Rak´ah. Asirefushe kiasi cha kuwatia uzito watu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22731/حكم-تطويل-الامام-ليلحق-الداخل-بالجماعة
  • Imechapishwa: 09/08/2023