Swali: Kuna mwanamke aliswali mara tu baada ya kusikia adhaana. Wakati alipofika katika Rak´ah ya mwisho akasikia waadhini wengine wawili wanaanza kuadhini. Ni ipi hukumu ya swalah yake?
Jibu: Ni lazima kwa muislamu kuwa mwangalifu juu ya dini yake na asiswali kabla ya wakati. Kwa sababu baadhi ya waadhini wanaweza kuadhini kabla ya wakati. Kwa ajili hiyo haitakiwi kudanganyika nao. Ikiwa inahusiana na tofauti ya dakika moja au mbili baina ya adhaana ya mwadhini wa kwanza na adhaana ya mwadhini wa pili, basi huhitaji kuirudia swalah yako. Hata hivyo katika unalazimika katika siku za mbele kusubiri mpaka ziwe nyingi adhaana za waadhini. Kuchukua tahadhari ni jambo la aula na bora zaidi.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/217)
- Imechapishwa: 17/04/2026
Swali: Kuna mwanamke aliswali mara tu baada ya kusikia adhaana. Wakati alipofika katika Rak´ah ya mwisho akasikia waadhini wengine wawili wanaanza kuadhini. Ni ipi hukumu ya swalah yake?
Jibu: Ni lazima kwa muislamu kuwa mwangalifu juu ya dini yake na asiswali kabla ya wakati. Kwa sababu baadhi ya waadhini wanaweza kuadhini kabla ya wakati. Kwa ajili hiyo haitakiwi kudanganyika nao. Ikiwa inahusiana na tofauti ya dakika moja au mbili baina ya adhaana ya mwadhini wa kwanza na adhaana ya mwadhini wa pili, basi huhitaji kuirudia swalah yako. Hata hivyo katika unalazimika katika siku za mbele kusubiri mpaka ziwe nyingi adhaana za waadhini. Kuchukua tahadhari ni jambo la aula na bora zaidi.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/217)
Imechapishwa: 17/04/2026
https://firqatunnajia.com/subiri-kidogo-usiharakie-kuswali/