Swali: Je, inaharibika swalah ya ambaye nguo yake inavuka kongo mbili za miguu?
Jibu: Maoni sahihi ni kwamba swalah yake haibatiliki. Hata hivyo ni mwenye kupata dhambi na anajiweka katika khatari ya kuadhibiwa. Ukiongezea ya kwamba anaburuta nguo kwa kiburi, basi adhabu yake ni kwamba Allaah hatomtazama siku ya Qiyaamah na wala hatomtakasa na atakuwa na adhabu yenye kuumiza. Na ikiwa anavaa nguo chini ya macho mawili ya miguu bila ya kiburi, anaadhibiwa kwa hali yoyote ile:
“Kile kikoi kilicho chini ya mafundo mawili ya miguu kiko ndani ya Moto.”[1]
Kwa ajili hiyo ikawa ni haramu kuvaa kanzu, suruwali na shali chini ya mafundo mawili ya miguu kwa hali zote. Hata hivyo adhabu yake ni kubwa zaidi pindi mtu anapoburuta kwa kiburi. Isitoshe ni miongoni mwa madhambi makubwa kwa sababu kumeambatana na matishio.
[1] al-Bukhaariy (5787).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/306-307)
- Imechapishwa: 18/04/2026
Swali: Je, inaharibika swalah ya ambaye nguo yake inavuka kongo mbili za miguu?
Jibu: Maoni sahihi ni kwamba swalah yake haibatiliki. Hata hivyo ni mwenye kupata dhambi na anajiweka katika khatari ya kuadhibiwa. Ukiongezea ya kwamba anaburuta nguo kwa kiburi, basi adhabu yake ni kwamba Allaah hatomtazama siku ya Qiyaamah na wala hatomtakasa na atakuwa na adhabu yenye kuumiza. Na ikiwa anavaa nguo chini ya macho mawili ya miguu bila ya kiburi, anaadhibiwa kwa hali yoyote ile:
“Kile kikoi kilicho chini ya mafundo mawili ya miguu kiko ndani ya Moto.”[1]
Kwa ajili hiyo ikawa ni haramu kuvaa kanzu, suruwali na shali chini ya mafundo mawili ya miguu kwa hali zote. Hata hivyo adhabu yake ni kubwa zaidi pindi mtu anapoburuta kwa kiburi. Isitoshe ni miongoni mwa madhambi makubwa kwa sababu kumeambatana na matishio.
[1] al-Bukhaariy (5787).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/306-307)
Imechapishwa: 18/04/2026
https://firqatunnajia.com/swalah-ya-mwanaume-chini-ya-vifundo-viwili-vya-miguu/