Swali: Je, inasihi swalah ya asiyekuwa na uwezo wa kuelekea Qiblah?
Jibu: Inasihi swalah yake. Dalili ya hilo ni maneno Yake Allaah (Ta´ala):
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]
لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا
“Allaah hakalifishi nafsi yoyote isipokuwa kwa kadiri ya uwezo wake.”[2]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ninayokukatazeni basi jiepusheni nayo na nikikuamrisheni jambo basi lifanyeni muwezavyo.”[3]
Asiyekuwa na uwezo halazimiki kuelekea Qiblah kutokana na kushindwa kwake. Kwa mfano mtu ni mgonjwa na hawezi kutikisika na pia hana mtu wa kumwelekeza Qiblah. Katika hali hii ataelekea kule alipoelekea, kwa sababu si muweza.
[1] 64:16
[2] 2:286
[3] al-Bukhaariy (7288) na Muslim (1337).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/411)
- Imechapishwa: 18/04/2026
Swali: Je, inasihi swalah ya asiyekuwa na uwezo wa kuelekea Qiblah?
Jibu: Inasihi swalah yake. Dalili ya hilo ni maneno Yake Allaah (Ta´ala):
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]
لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا
“Allaah hakalifishi nafsi yoyote isipokuwa kwa kadiri ya uwezo wake.”[2]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ninayokukatazeni basi jiepusheni nayo na nikikuamrisheni jambo basi lifanyeni muwezavyo.”[3]
Asiyekuwa na uwezo halazimiki kuelekea Qiblah kutokana na kushindwa kwake. Kwa mfano mtu ni mgonjwa na hawezi kutikisika na pia hana mtu wa kumwelekeza Qiblah. Katika hali hii ataelekea kule alipoelekea, kwa sababu si muweza.
[1] 64:16
[2] 2:286
[3] al-Bukhaariy (7288) na Muslim (1337).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/411)
Imechapishwa: 18/04/2026
https://firqatunnajia.com/je-swalah-ni-sahihi-mtu-asipoweza-kuelekea-qiblah/