Swali: Je, ipo njia fulani ya kujua ni wapi kipo Qiblah?
Jibu: Ndio ipo. Ikiwa mtu yuko jangwani anaweza siku zote kutazama jua, mwezi na nyota. Jua huchomoza mashariki na huzama magharibi. Kwa hivyo ikiwa mtu yuko magharibi mwa Makkah, basi ataelekea mashariki, na ikiwa yuko mashariki ya Makkah, basi ataelekea magharibi. Ikiwa yuko kaskazini mwa Makkah, basi ataelekea kusini, na ikiwa yuko kusini mwa Makkah, basi atalekea kaskazini. Hii ni alama kubwa.
Ikiwa atafanya bidii yake kisha baadaye ikambainikia kuwa amekosea Qiblah, basi hatorudia swalah ikiwa yuko maeneo ambayo hawezi kuwauliza watu. Hii leo Allaah amewafanya wepesi wa kujua ni wapi kilipo Qiblah kwa kutumia dira. Kwa hivyo ikiwa mtu anataka kusafiri mahali fulani basi aende na dira hii ili atambue atachofanya.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/417)
- Imechapishwa: 18/04/2026
Swali: Je, ipo njia fulani ya kujua ni wapi kipo Qiblah?
Jibu: Ndio ipo. Ikiwa mtu yuko jangwani anaweza siku zote kutazama jua, mwezi na nyota. Jua huchomoza mashariki na huzama magharibi. Kwa hivyo ikiwa mtu yuko magharibi mwa Makkah, basi ataelekea mashariki, na ikiwa yuko mashariki ya Makkah, basi ataelekea magharibi. Ikiwa yuko kaskazini mwa Makkah, basi ataelekea kusini, na ikiwa yuko kusini mwa Makkah, basi atalekea kaskazini. Hii ni alama kubwa.
Ikiwa atafanya bidii yake kisha baadaye ikambainikia kuwa amekosea Qiblah, basi hatorudia swalah ikiwa yuko maeneo ambayo hawezi kuwauliza watu. Hii leo Allaah amewafanya wepesi wa kujua ni wapi kilipo Qiblah kwa kutumia dira. Kwa hivyo ikiwa mtu anataka kusafiri mahali fulani basi aende na dira hii ili atambue atachofanya.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/417)
Imechapishwa: 18/04/2026
https://firqatunnajia.com/je-ipo-njia-fulani-ya-kujua-ni-wapi-kipo-qiblah/