Msafiri hajui ni wapi Qiblah kipo

Swali: Ni kipi msafiri afanye ikiwa hajui ni wapi Qiblah kipo?

Jibu: Atajitahidi ule upande anafikiria uko karibu zaidi na Qiblah na aswali kwa kuelekea huko. Akifanya hivo na akamcha Allaah vile awezavyo, basi hatohitajia kuirudia swalah yake endapo itabaini kuwa amekosea mwelekeo. Allaah (Ta´ala) amesema:

لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا

“Allaah hakalifishi nafsi yoyote isipokuwa kwa kadiri ya uwezo wake.”[1]

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[2]

وَلِلَّـهِ الْمَشْرِقُ وَالْمَغْرِبُ ۚ فَأَيْنَمَا تُوَلُّوا فَثَمَّ وَجْهُ اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ وَاسِعٌ عَلِيمٌ

”Mashariki na Magharibi ni milki ya Allaah. Hivyo basi popote mnapogeuka kuna uso wa Allaah. Hakika Allaah ni Mwenye wasaa, Mjuzi wa yote.[3]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ninayokukatazeni basi jiepusheni nayo na nikikuamrisheni jambo basi lifanyeni muwezavyo.”[4]

[1] 2:286

[2] 64:16

[3] 2:115

[4] al-Bukhaariy (7288) na Muslim (1337).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/417-418)
  • Imechapishwa: 18/04/2026