Hatusomi Qur-aan kwa njia ya kuizingatia na kuwaidhika na yaliyomo ndani. Waislamu wengi wanasoma Qur-aan kwa ajili ya kutafuta baraza zake na kutaka thawabu tu. Linalotakikana ni sisi kusoma Qur-aan kwa mazingatio na kwa ajili ya kuwaidhika na yaliyomo ndani. Allaah (Ta´ala) amesema:

كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ مُبَارَكٌ

“Kitabu Tumekiteremsha kwako chenye baraka… ”

Huu ni ujira.

لِّيَدَّبَّرُوا آيَاتِهِ

”… ili wapate kuzingatia kwa makini Aayah zake… ”

Haya ndio matunda.

وَلِيَتَذَكَّرَ أُوْلُوا الْأَلْبَابِ

”… na ili wapate kukumbuka wale wenye akili.”[1]

[1] 38:29

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/142)
  • Imechapishwa: 29/04/2024