42. Ukitaka kujua kuwa Jahmiy hathibitishi ujuzi wa Allaah

Ukitaka kujua kuwa Jahmiy hathibitishi ujuzi wa Allaah, mwambie kuwa Allaah (Ta´ala) anasema:

وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ

“… na  wala hawakizunguki chochote katika elimu Yake isipokuwa kwa akitakacho.”[1]

لَّـٰكِنِ اللَّـهُ يَشْهَدُ بِمَا أَنزَلَ إِلَيْكَ ۖ أَنزَلَهُ بِعِلْمِهِ

”Lakini Allaah anayashuhudia aliyoyateremsha kwako; ameyateremsha kwa ujuzi Wake.”[2]

فَإِلَّمْ يَسْتَجِيبُوا لَكُمْ فَاعْلَمُوا أَنَّمَا أُنزِلَ بِعِلْمِ اللَّـهِ

”Wasipokujibuni, basi tambueni ya kwamba hakika imeteremshwa kwa ujuzi wa Allaah.”[3]

إِلَيْهِ يُرَدُّ عِلْمُ السَّاعَةِ ۚ وَمَا تَخْرُجُ مِن ثَمَرَاتٍ مِّنْ أَكْمَامِهَا وَمَا تَحْمِلُ مِنْ أُنثَىٰ وَلَا تَضَعُ إِلَّا بِعِلْمِهِ ٍ

”Kwake pekee unarudishwa utambuzi wa Saa; na hayatoki matunda yoyote kutoka mafumbani mwake na hakuna mwanamke yeyote anayebeba mimba na wala hazai isipokuwa kwa utambuzi Wake.”[4]

Muulize kama yeye anathibitisha elimu ya Allaah ambayo kwayo amemtunuku elimu na hoja. Akisema kuwa Hajui, anakuru, Akisema kuwa Allaah anayo elimu yenye kuzuka, anakufuru pia. Kwa sababu maana yake ni kwamba kuna kipindi ambapo Allaah alikuwa hajui mpaka ikamzukia elimu, akajua baada ya hapo. Na akisema kuwa Allaah anayo elimu na haikuumbwa na wala si yenye kuzuka, basi atakuwa amejirejea kikamilifu kutokana na maoni yake na amesema kama walivosema Ahl-us-Sunnah[5].

[1] 2:255

[2] 4:166

[3] 11:14

[4] 41:47

[5] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:

”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 157
  • Imechapishwa: 29/04/2024