Swali: Tumewaona baadhi ya ambao wanafanya Tamyi´ utu wa ki-Sunniy wanakuja na kanuni ambazo mara nyingi zimewafanya wanafunzi kutumbukia katika fikira za kuangamiza na hisia zinazotekanyara. Wanawasikiliza watoa mawaidha, waalimu na wanachuoni wote pasi na kujali mirengo yao. Wanafanya hivo kujengea kanuni isemayo:

“Tunawasikiliza wote kisha tunachuja.”

Ni upi usahihi wa maneno haya khaswa kwa kuzingatia kwamba maneno yangu yanawahusu watu ambao sio wanafunzi?

Jibu: Unawazungumzia wanafunzi?

Muulizaji: Wanafunzi na wasiokuwa wanafunzi.

Jibu: Jibu langu fupi juu ya hili ni kwamba wafanye hivo ikiwa kweli wanajiona kwamba wanao uwezo wa kuchuja.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (512)
  • Imechapishwa: 03/10/2020