Swali: Je, kunaingia katika kugusa msahafu pasi na wudhuu´ endapo mtu atagusa kifuniko cha nje cha msahafu na makaratasi ambayo hayana Aayah lakini hata hivyo makaratasi hayo ni ya msahafu?

Jibu: Asiuguse isipokuwa nyuma ya kizuizi. Kifuniko cha msahafu ni katika msahafu. Lakini ni hakuna neno endapo kifuniko hicho anachogusa ni nyongeza juu ya kile kifuniko cha msahafu. Wako watu wengine ambao wanauweka ndani ya mfuko au nyuma ya vifuniko vya mikono, jambo ambalo ni la sawa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (17)
  • Imechapishwa: 03/10/2020