Sifa mbili kuu za Allaah ambazo sifa zingine zote zinarejea kwazo

Baadhi ya wanachuoni wamesema kuwa majina haya mawili: al-Hayy al-Qayyuum (Aliye hai na Mwenye kuyasimamia mambo) ndio jina kuu la Allaah. Muhimili wa majina yote mazuri yanarudi kwenye majina haya mawili na maana yake inarudi kwenye majina hayo.

Sifa zote za kimatendo zinarudi kwenye sifa ya uhai (al-Hayy). Allaah (Ta´ala) ana uhai mkamilifu. Sifa zote kamilifu zinarejea katika sifa hiyo.

Mwenye kuyasimamia mambo yote (al-Qayyuum) ni dalili inayoonyesha kujitosheleza Kwake (Subhaanahu wa Ta´ala). Hamuhitajii yeyote kwa hali yoyote ile. Ni mkamilifu tokea kale. Ni sifa inayotoa dalili kuonyesha kuwa Mola ni mkamilifu, ukamilifu wa nguvu Zake, uwezo Wake na kuendelea hivyo daima na milele. Amejitosheleza na wengine ndio wenye kumuhitajia (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/67)
  • Imechapishwa: 31/05/2020