Mushabbihah wamefanana na manaswara

Mwenye kumfananisha Allaah na viumbe Wake na kuamini kuwa Allaah anafanana na viumbe, mtu huyo hakika hamwabudu Allaah. Anaabudu sanamu alilolitengeneza [mwenyewe]. Ni kufuru. Watu hawa ni wenye kuabudu masanamu na hawamuabudu Allaah.

Mwenye kumfananisha Allaah na viumbe Wake ameshabihiana na manaswara. Kama jinsi Allaah hafanani na yeyote katika viumbe Wake, basi vilevile hafananishwi na yeyote katika viumbe Wake.

Madhehebu ya Mushabbihah na madhehebu ya manaswara. Mushabbihah wamemfananisha Allaah na viumbe Wake na kusema kuwa Allaah ni kama viumbe Wake. Manaswara wamewafananisha viumbe na Mola na kusema kuwa ´Iysaa ni mwana wa Allaah. Wote ni wafananishaji.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/64)
  • Imechapishwa: 01/06/2020