Si wakeze Mtume wala jamaa zake wa karibu hakuna aliyekingwa na kukosea

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Ee ´Aaishah! Hakika nimefikiwa na tetesi zako. Ukiwa huna hatia basi Allaah atakutakasa. Na ikiwa umetenda dhambi, basi mtake Allaah msamaha na tubu Kwake.”[1]

Hadiyth ni dalili ya kukata kabisa dhidi ya yule ambaye amezua imani ya kwamba wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wamekingwa na kukosea kutokana na kwamba Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيُذْهِبَ عَنكُمُ الرِّجْسَ أَهْلَ الْبَيْتِ وَيُطَهِّرَكُمْ تَطْهِيرًا

“Hakika si vyenginevyo Allaah anachotaka ni kukuondosheeni maovu, watu wa nyumba, na akutakaseni mtakaso ukweli wa kuwatakasa.”[2]

Ima ni mjinga au anajifanya kuwa ni mjinga juu ya matakwa katika Aayah sio ya kilimwengu ambayo ni lazima yatokee. Matakwa katika Aayah ni ya kidini ambayo ndani yake kuna kupenda na kuridhia. Vinginenvyo Shiy´ah wanaweza kutumia Aayah hiyohiyo kama dalili juu ya kwamba maimamu wa Nyumba wote wamekingwa na kukosea na khaswa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh). Hiki ni kitu ambacho ameghafilika nacho mzushi ingawa anadai kuwa ni Salafiy! Ndio maana Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

”Aayah ya kutwahirisha haifahamishi kuwa wafuasi wa karibu wa Nyumba kwamba wametwahirishwa na kusafishwa. Hata hivyo Aayah inawaamrisha kufanya yale yanayopelekea katika kutwahirishwa… Imethibiti kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimzungusha ´Aliy, Faatwimah, al-Hasan na al-Husayn ndani ya kitambara na akasema:

”Ee Allaah! Hawa ndio watu wa nyumbani kwangu! Waondoshee uchafu na uwatwahirishe kikamilifu.”[3]

Kuna dalili ya kwamba yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakueleza kuwa wamekwishatwahirishwa. Vinginevyo angelikuwa anamsifu na kumshukuru Allaah na si kuishilia peke yake kumuomba Allaah.”[4]

[1] Muslim.

[2] 33:33

[3] Muslim

[4] Minhaaj-us-Sunnah (4/22-24).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (4/529-530)
  • Imechapishwa: 04/08/2020