Endapo vijana wetu wangejishughulisha na msingi huu ipasavyo basi wangelisalimika kutumbukia katika katika mambo mengi ambayo sio fani yao na ambayo kujishughulisha nayo ni kupoteza muda. Mfano wa mambo hayo wanayojishughulisha nayo ni kufuatiliafuatilia mambo ya siasa, kuwalingania watu wote kuyafahamu mambo ya siasa na mengineyo. Mambo haya na mfano wake hayamuhusu mwanafunzi. Mambo haya yanawahusu watawala au manaibu wao. Pindi makundi ya vijana walipojivugumiza na wakajiweka nafsi zao katika nafasi za watawala ukabainika ujinga wao, ukadhihiri upotevu wao na kutekeleza kwao kukaonekana katika masuala haya. Kwa sababu kile wanachokitegemea ni vile visa vya uongouongo kwenye magazeti ya kigeni na idhaa za kikafiri. Hayo ndio wanayoyategemea. Wanajenga hukumu zao juu yake, kama mambo yalivyo katika vita vya Ghuba. Baadhi yao walitegemea visa na idhaa kama hizi. Matokeo yake wakajitenga mbali na waislamu, wakaingiza woga ndani ya mioyo yao, wakasambaratisha na kutenganisha umoja waliokuwa nao. Mategemezi haya juu ya visa na juu ya idhaa za kigeni ndio kilele cha mwisho walichonacho juu ya kile wanachokiita “Usuwl Fiqh-il-Waaqiy´”.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Usuwl-ud-Da´wah as-Salafiyyah, uk. 34-35
  • Imechapishwa: 04/08/2020