Shaykh amesema… Lakini ni kipi Shaykh alichosema?

Swali: Ni ipi hukumu ya kutoa fatwa kutokana na yale aliyosikia mtu kutoka kwa wanazuoni?

Jibu: Suala hili lina tatizo[1]. Dalili ya kwanza juu ya tatizo lake ni tetesi hizi zinazosema kuwa mimi nakataza kutufu Nyumba kwa wale ambao ni wakazi wa Makkah. Ukweli wa mambo ni kwamba suala hili linatatiza. Baadhi ya watu husikia mambo na wasiyafahamu vizuri kisha wanawaendea watu na kusema kwamba fulani amesema kadhaa na kadhaa. Wengine huuliza kwa njia inayomfanya yule mtoa fatwa kuelewa vyengine na matokeo yake mtoa fatwa anajibu kutokana na ufahamu wake na hivyo mtu huyo anayapokea kwa ufahamu mwingine na hivyo kunatokea makosa. Lakini mtu akimsikia mwanachuoni anasema kitu na akakihakikisha, basi inafaa kwake kumnakili. Lakini kama anayo mashaka, basi ni lazima kwake kuhakikisha kwanza.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/shaykh-amesema/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=8tuCLo7TNwQ
  • Imechapishwa: 29/05/2021